Uturuki imelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea kwenye ufukwe wa Bondi Beach mjini Sydney, Australia, lililosababisha vifo vya takriban watu 12 na kujeruhi wengine 29. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilitoa rambirambi kwa familia za waathiriwa na watu wa Australia, huku ikiwatakia majeruhi kupona haraka.
Ankara ilisisitiza msimamo wake thabiti dhidi ya ugaidi wa aina zote na ikathibitisha kujitolea kwake kuendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, hususan Australia, katika mapambano dhidi ya tishio la ugaidi duniani.
CHANZO: TRT Afrika













