Serikali ya Uturuki imesema inaandaa mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot air defence system katika eneo la mashariki mwa nchi ili kuimarisha usalama wa anga lake kufuatia mvutano unaoendelea katika eneo hilo.
Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilisema hatua hiyo inafanywa kwa ushirikiano na NATO, huku mfumo huo ukiandaliwa katika mji wa Malatya, ambako pia kuna kituo cha rada cha tahadhari ya mapema kilichowekwa na NATO tangu mwaka 2012.
Hatua hiyo imekuja baada ya mifumo ya ulinzi ya NATO kudungua kombora lililorushwa kutoka Iran kuelekea Uturuki, ikiwa ni tukio la pili ndani ya wiki moja ambapo makombora ya Iran yaliingia anga ya Uturuki.
CHANZO: TRT Afrika














