Serikali ya Benin imethibitisha kuwa watu kadhaa, wakiwemo wanajeshi na raia, wameuawa wakati wa kukabiliana na jaribio la mapinduzi lililotokea mwishoni mwa wiki. Waasi walijaribu kumvua madarakani Rais Patrice Talon na kuwataka nyara viongozi wa juu wa kijeshi. Mapigano makali yalizuka katika makazi ya rais na katika kambi ya kijeshi ya Togbin. Baadhi ya waasi wamekamatwa huku wengine wakisakwa. Benin ilipata msaada wa kijeshi kutoka Nigeria na ECOWAS katika kuudhibiti uasi huo, na serikali imetangaza kuwa operesheni imefanikiwa na maeneo yote yamerejeshwa chini ya udhibiti wa jeshi.
CHANZO: TRT Afrika














