Serikali ya Kenya imethibitisha kuwa watu 62 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa mamlaka, nchi hiyo iko katika kipindi cha mwanzo cha msimu wa mvua ndefu, hali ambayo inaweza kusababisha mafuriko zaidi na uharibifu wa mali.
Timu za uokoaji zinaendelea kufanya operesheni katika maeneo yaliyoathirika huku serikali ikitoa msaada kwa familia zilizopoteza makazi yao.
CHANZO: TRT Afrika














