Watu wasiopungua 25 wameokolewa na wengine 25 hawajulikani waliko siku mbili baada ya boti lililokuwa limebeba watu karibu 50 katika Jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto, idara ya huduma za dharura imesema siku ya Jumanne.
Mamlaka ya Taifa ya Masuala ya Dharura (NEMA) inasema watu 25 walikuwa bado hawajulikani waliko au pengine wanasemekana kufariki. Hakuna miili yoyote iliyopatikana kufikia Jumanne asubuhi, mamlaka hiyo imesema.
Chombo hicho, ambacho kilikuwa kilikuwa na abiria wanawake, watoto, na pikipiki kuelekea soko la Goronyo, sehemu ya mazao katika eneo hilo, lilipindukia Jumapili, maafisa wanasema.














