Katika mabadiliko ya ghafla ya baraza la mawaziri, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewafuta kazi Waziri wa Afya Elijah Muchima na Waziri wa Kukuza Biashara Ndogo na za Kati Elias Mubanga.
Taarifa ya Ikulu imesema mabadiliko hayo yametekelezwa kwa mujibu wa Katiba ya Zambia, na Rais amewashukuru mawaziri hao kwa huduma yao.
Elijah Muchima aliteuliwa Julai 2024 kuchukua nafasi ya Sylvia Masebo kama Waziri wa Afya, lakini sasa ameondolewa kazini bila sababu rasmi kutolewa. Rais Hichilema amesema walioteuliwa kuchukua nafasi hizo watatangazwa kwa wakati muafaka.
CHANZO: TRT Afrika














