Watu wasiopungua watatu wauawa, 34 wajeruhiwa wakati Israel ikishambulia mji mkuu wa Syria

Watu wasiopungua watatu wameuawa na wengine 34 kujeruhiwa baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi ya angani katika mji mkuu wa Syria Damascus siku ya Jumatano.

Newstimehub

Newstimehub

16 Julai, 2025

de75b8bab65a6be31be4ff4aa6a760d3c56d78e89e6328551d025c98e97991ae

Watu wasiopungua watatu wameuawa na wengine 34 kujeruhiwa siku ya Jumatano baada ya jeshi la Israel kufanya mashambulizi ya angani katika mji mkuu wa Syria, Damascus, wizara ya afya imesema.

Shirika la habari la taifa SANA linasema ndege za kivita zimeshambulia eneo la Ikulu ya Rais, linalojulikana kama Qasr al-Shaab, katika mji mkuu.

Jeshi la Israel limethibitisha kuhusu mashambulizi ya angani na kuita shambulizi katika ikulu ya Rais kama “shambulizi la onyo.”

Video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha wakati ambao mashambulizi ya Israel yalivyofanyika Damascus, huku moshi ukiwaka.

Maeneo mengi yameshambuliwa Syria

Ndege za kivita za Israel pia zilishambulia katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Daraa na mji wa Qatana, kulingana na SANA.

Mashambulizi hayo yamekuja muda mfupi baada ya Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz kuapa “kuikabili vikali” Syria.

“Mashambulizi makali yameanza,” Katz alisema wakati akionesha video ya mtangazaji wa Televisheni ya Syria ikitetemesha kituo hicho wakati wa matangazo.

Kulingana na Shirika la habari la umma la Israel KAN, linasema jeshi la Israel limeshambulia maeneo karibu 160 nchini Syria tangu usiku wa jana, mengi yakiwa katika mji wa kusini wa Suwayda.

Mapigano ya siku kadhaa

KAN inasema mkuu wa majeshi Eyal Zamir ameagiza vikosi viondolewe Gaza na kupelekwa katika milima iliyokaliwa ya Golan.

Shirika hilo, likitaja vyanzo vya kiusalama, kuwa jeshi la Israel linajiandaa kwa mapigano ya siku kadhaa nchini Syria.

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya angani katika maeneo ya Syria tangu Jumanne, hasa eneo la Suwayda, katika hatua ya hivi karibuni ya kukiuka uhuru wa nchi kwa madai ya kuwalinda watu wa madhehebu ya Druze nchini Syria.

Mashambulizi yanafanyika wakati wanajeshi wa Syria wamepelekwa kwenye mkoa huo kurudisha hali ya usalama na kulinda raia na mali zao, kufuatia mapigano kati ya madhehebu ya Druze wenye silaha na makundi ya mabedui na kusababisha vifo vya watu 30.

Siku ya Jumatano, wizara ya mambo ya ndani ya Syria ilitangaza makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano na viongozi wa Druze huko Suwayda.