Afrika

Zohran Mamdani mazaliwa Uganda achaguliwa kuwa Meya wa mji wa New York

Zohran Mamdani,mwenye umri wa miaka 34 na anayejitambulisha kama msoshalisti, amechaguliwa kuwa Meya wa mji wa New York.

Newstimehub

Newstimehub

5 Novemba, 2025

1762326939778 wmb8v9 2c18532ce48008d676aef43e0df13937166d0c1e057c8538f9cd3b3e747c20fd

Zohran Mamdani amewashinda gavana wa zamani Andrew Cuomo na mgombea wa Republican Curtis Sliwa.

Mamdani, mzaliwa wa Uganda mwenye asili ya Kihindi, amekuwa Meya wa kwanza Mwislamu na mwenye asili ya Asia Kusini katika historia ya mji huo.

Kampeni yake ilijikita katika masuala ya gharama za maisha, akihaidi kusimamisha ongezeko la kodi ya nyumba, kutoa usafiri wa umma bure, na kuongeza kodi kwa matajiri.

Licha ya kushambuliwa vikali na Rais Donald Trump, matajiri wakubwa na makundi yanayounga mkono Israel, mtindo wake wa kampeni unaotegemea wananchi wa kawaida uliwapendeza wapiga kura, na kuashiria mwelekeo mpya wa mrengo wa kushoto ndani ya Chama cha Democratic.