Umoja wa Mataifa umeitaka Eritrea na Ethiopia kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa Algiers uliosainiwa miaka 25 iliyopita, uliokomesha rasmi vita vya mpaka vilivyodumu kati ya 1998 na 2000 na kuua maelfu ya watu. UN imeonya kuwa dalili za mvutano unaojitokeza upya zinaweza kuhatarisha amani na utulivu wa eneo la Pembe ya Afrika.
Katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa ulisisitiza umuhimu wa kuheshimu mipaka iliyokubaliwa, mamlaka ya mataifa na kuendeleza uhusiano wa ujirani mwema. UN pia imehimiza pande zote mbili kuendelea kushirikiana na washirika wa kikanda na kimataifa ili kudumisha amani na kuendeleza maendeleo kwa manufaa ya raia wa nchi hizo.
CHANZO: TRT Afrika














