Benin imewakamata karibu watu 30, wengi wao wakiwa wanajeshi, kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mapema mwezi huu. Waliokamatwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhaini, mauaji na kuhatarisha usalama wa taifa, huku wakizuiliwa kabla ya kesi baada ya kufikishwa mbele ya mwendesha mashtaka mjini Cotonou.
CHANZO: TRT Afrika












