Marekani imeishutumu Rwanda kwa kuchochea mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo licha ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani Washington. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema Rwanda imetoa msaada wa kijeshi, vifaa na mafunzo kwa waasi wa M23, madai ambayo Kigali imeendelea kuyakanusha, huku hali ya usalama katika mkoa wa Kivu Kusini ikiendelea kuzorota.
CHANZO: TRT Afrika














