Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa mahindi tani 500 kwa Msumbiji kufuatia mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua kubwa. Msaada huo ulikabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje Mahmoud Thabit Kombo kwa ujumbe wa Msumbiji.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Kombo alisema msaada huo umetolewa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kama ishara ya mshikamano na huruma kwa wananchi wa Msumbiji waliokumbwa na janga hilo.
CHANZO: TRT Afrika














