Serikali ya Nigeria imeanza juhudi za kuwarejesha kwa hiari raia wake kutoka Afrika Kusini huku maandamano dhidi ya wahamiaji yakiongezeka katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Bianca Odumegwu-Ojukwu, amesema serikali tayari imeanza kukusanya taarifa za Wanigeria wanaotaka kurejea nyumbani.
Hatua hiyo imekuja baada ya hofu ya usalama kuongezeka miongoni mwa wahamiaji kutokana na maandamano ya kupinga wageni yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
CHANZO: TRT Afrika

















