Wamisri 14 wafariki baada ya boti la wahamiaji kuzama Crete
“Tunatoa wito kwa raia wa Misri kutohadaiwa na mitandao ya uhamiaji haramu,” ilisema Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.
Newstimehub
16 Desemba, 2025
Wamisri wasiopungua 14 wamefariki baada ya boti la wahamiaji kuzama karibu na bandari ya kisiwa cha Crete nchini Ugiriki. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema boti hilo lilikuwa limebeba wahamiaji 34 kutoka mataifa mbalimbali na liliondoka kuelekea Ugiriki Disemba 7, huku ikionya dhidi ya hatari za uhamiaji haramu.