Mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini Kenya imesababisha mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu takriban 81 mwezi huu. Maeneo mengi yameathirika huku wakazi wakilazimika kuvuka maji wakibeba mali zao na wengine kuokolewa kwa kutumia maboti.
Katika kaunti ya Kisumu, mafuriko yameharibu mashamba makubwa na kufukia vijiji, huku familia zaidi ya 3,000 zikikosa makazi katika eneo la Nyakach. Mamlaka zimeonya kuwa mvua itaendelea, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.
CHANZO: TRT Afrika














