Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, wakijadili uhusiano wa nchi zao pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.
Katika mazungumzo hayo, Erdogan alisisitiza kuwa Uturuki inaipa kipaumbele kuimarisha uhusiano wake na Canada, hasa katika sekta muhimu kama nishati, ulinzi na usafiri wa anga.
Pia alibainisha kuwa nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana kwa karibu zaidi katika kukuza amani na utulivu wa kikanda, kutokana na misingi yao ya pamoja katika diplomasia ya kimataifa.
CHANZO: TRT Afrika














