Michezo Afrika

Simba Yatwaa Kombe la Muungano Kwa Bao la Dakika za Mwisho.

Simba SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Young Africans SC kupitia bao la Selemani Mwalimu dakika za nyongeza.

Newstimehub

Newstimehub

30 Aprili, 2026

Screenshot 20260430 074359 Instagram

Simba SC imeibuka bingwa wa Kombe la Muungano baada ya kuifunga Young Africans SC kwa bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Amaan Complex,mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku timu zote zikionesha ubora mkubwa kuanzia dakika za mwanzo. Yanga walionekana kuwa na umiliki mzuri wa mpira, huku Simba wakitegemea zaidi mashambulizi ya kushtukiza yaliyoleta hatari mara kadhaa langoni.

Dakika 90 za kawaida zilimalizika bila mabao, jambo lililolazimisha mechi kuingia katika muda wa nyongeza. Ndipo shujaa wa Simba, Selemani Mwalimu, alipofunga bao la ushindi katika dakika za jioni za extra time, akitumia vyema nafasi iliyopatikana ndani ya eneo la hatari,bao hilo liliamsha shangwe kubwa kwa mashabiki wa Simba waliokuwa uwanjani, huku wachezaji wa Yanga wakionekana kusikitishwa na matokeo hayo baada ya kupambana kwa muda mrefu.

Ushindi huo unaipa Simba taji muhimu na kuongeza morali kuelekea mechi ijayo dhidi ya wapinzani hao hao katika NBC Premier League tarehe 3, ambapo ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi.

Chanzo:Azam sport