Ulimwengu

Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri wa Fedha wa Israel

Hati hizo, pia zinajumuisha kukamatwa kwa maofisa watatu wa kijeshi wa Israel na wanasiasa wawili.

Newstimehub

Newstimehub

19 Mei, 2026

b6ebb5f81a468720885b28ce2e23edbba37ccddc0577d464516194e6a535a699

Waziri wa Fedha wa Israel Bezalel Smotrich, amesema kuwa amejulishwa kuhusu mpango wa kumkamata kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), siku ya Jumanne.

“Usiku wa jana nilijulishwa kuhusu mkakati huo wa kunikamata,” alisema Smotrich.

Kulingana na Smotrich, mpango huo ni sawa na “kutangaza vita” na jaribio la kuongeza vikwazo dhidi ya Israel.

 “Hatutokubali unafiki wa aina hii dhidi ya Israel,” aliongeza.

Siku ya Jumapili, gazeti la kila siku la nchini Israel Haaretz, lilikinukuu chanzo kimoja cha kidiplomasia, kikisema kuwa mwendesha mashtaka wa ICC analenga kutoa hati za kukamatwa kwa maofisa kadhaa wa Israel.

Hati hizo zinajumuisha kukamatwa kwa maofisa watatu wa kijeshi wa Israel na wanasiasa wawili.