Ulimwengu

Mojtaba Khamenei amesema madini ya urani ya Iran yatabaki nchini humo

Rais Donald Trump ameapa kutoruhusu Iran kuwa na madini hayo au kuiruhusu kuwa na silaha za nyuklia.

Newstimehub

Newstimehub

22 Mei, 2026

2026 05 21t102751z 1032983550 rc2v4lalz6uh rtrmadp 3 iran crisis nuclear

Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei ametoa agizo ya kwamba madini ya urani ya Iran, ambayo yamefikia kiwango kinachohitajika kutengeneza silaha, yasipelekwe nje ya nchi, kwa mujibu wa vyanzo viwili vya juu vya Iran.

Hatua hiyo inaifanya Iran kuwa na msimamo mkali zaidi kuhusu moja ya masharti makuu ya Marekani katika mazungumzo ya amani.

Uamuzi wa Mojtaba Khamenei unaweza kumkasirisha zaidi Rais wa Marekani, Donald Trump, na kufanya mazungumzo ya kumaliza vita vinavyoendeshwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa magumu zaidi.

Rais Donald Trump ameapa kutoruhusu Iran kuwa na madini hayo au kuiruhusu kuwa na silaha za nyuklia.

Moja ya mapendekezo ya Marekani katika mazungumzo hayo ya amani ni urani ya Iran kuondolewa nchini humo na kupelekwa nchi nyengine ikiwemo Marekani