Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amewasili nchini Urusi kwa mazungumzo ya ngazi ya juu na Rais Vladimir Putin huku juhudi za kidiplomasia kati ya Iran na Marekani zikiwa katika hali ya sintofahamu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran IRNA, Araghchi aliwasili mapema Jumatatu kwa lengo la kukutana na Putin na kufanya mazungumzo kuhusu hali ya sasa ya mgogoro unaohusisha Tehran na Washington.
Kremlin pia imethibitisha kuwa rais wa Urusi anatarajiwa kumpokea Waziri huyo wa Iran katika mazungumzo muhimu kuhusu hali ya kikanda na juhudi za amani.
CHANZO: TRT Afrika














