Rais Donald Trump wa Marekani, amesema kuwa kwa sasa, nchi yake ina udhibiti kamili wa Mlango Bahari wa Hormuz.
Akizungumza siku ya Jumatano, Trump alisema kuwa Marekani itaendelea kuwepo katika njia hiyo muhimu ya kusafirisha bidhaa za mafuta duniani.
“Marekani ina udhibiti kamili wa Mlango Bahari wa Hormuz, nadhani tutaendelea kuudhibiti,” aliandika Trump kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Truth Social.
Kulingana na kiongozi huyo, uwezo wa kijeshi wa Iran umedhibitiwa vya kutosha, huku wanajeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) wakisambaratika na kukimbia.
Trump alidai kuwa uchumi wa Iran upo katika hali ya kuporomoka.
“Wanachojivunia nacho habari potofu na mfumuko wa bei uliofikia asilimia 100 na hali inazidi kuwa mbaya kwao,” Trump alidai.

















