Ulimwengu

Iran yawataka raia wake kupunguza matumizi ya petroli

Wiki iliyopita, Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Jafar Ghaempanah, alikaririwa akisema kuwa, uzalishaji wa ndani wa petroli haukuwa wa kuridhisha.

Newstimehub

Newstimehub

1 Septemba, 2026

d14dc4ec 91bb 4887 a5b8 3f09d5c4b4de 1788281007279

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf  amewataka raia wa nchi hiyo, kupunguza matumizi ya nishati ya petroli.

Ghalibaf, ambaye pia anahusika katika upatinishi wa vita vya eneo la Mashariki ya Kati, ametoa raia hiyo, wakati taifa hilo, likikabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta.

“Hakuna shaka kuwa tatizo lililopo halitokani na wananchi wetu, bali viwanda vyetu,” alisema Mohammad Bagher Ghalibaf katika hotoba yake kwa njia ya televisheni.

Hayo yanajiri wakati Marekani imeweka zuio kwenye bandari za Iran, kama kisasi kwa kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz, ambao huusika na usafirishwaji wa bidhaa muhimu kama vile mafuta na gesi.

Wiki iliyopita, Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Jafar Ghaempanah, alikaririwa akisema kuwa, uzalishaji wa ndani wa petroli haukuwa wa kuridhisha.