Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf amewataka raia wa nchi hiyo, kupunguza matumizi ya nishati ya petroli.
Ghalibaf, ambaye pia anahusika katika upatinishi wa vita vya eneo la Mashariki ya Kati, ametoa raia hiyo, wakati taifa hilo, likikabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta.
“Hakuna shaka kuwa tatizo lililopo halitokani na wananchi wetu, bali viwanda vyetu,” alisema Mohammad Bagher Ghalibaf katika hotoba yake kwa njia ya televisheni.
Hayo yanajiri wakati Marekani imeweka zuio kwenye bandari za Iran, kama kisasi kwa kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz, ambao huusika na usafirishwaji wa bidhaa muhimu kama vile mafuta na gesi.
Wiki iliyopita, Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Jafar Ghaempanah, alikaririwa akisema kuwa, uzalishaji wa ndani wa petroli haukuwa wa kuridhisha.

















