Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, amegomea wito uliotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani, wa kutaka mataifa mbalimbali kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
“Huo ndio msimamo wetu,” alisema Wadephul siku ya Jumatano, akisisitiza kuwa Ujerumani itaendelea kuiunga mkono ICC.
Kauli yake, inakuja siku moja baada ya rais Trump, kuiita ICC, “kikundi cha watu wabaya”, wakati akifungua majadiliano ndani ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akiyataka mataifa mbalimbali duniani, kujitoa kwenye mahakama hiyo.
“Hadi sasa, sielewi hoja yake,” alisema Wadephul.
Kulingana na Wadephul, ICC inaendelea kuwa taasisi muhimu ya kulinda haki za kibinadamu na kuwawajibisha wale wote wanaokiuka haki hizo.
“Tumejionea wenyewe, namna maamuzi ya ICC yalivyoshughulikia udhalimu na ukiukwaji wa haki za binadamu, katika nchi za Kibalkani,” aliongeza.

















