Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewataka viongozi ulimwenguni kulichukulia suala la mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa ‘umakini zaidi’.
Guterres ametoa wito huo siku ya Jumatatu wakati macho na masikio yakielekezwa jijini Antalya, Uturuki kwa ajili ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, maarufu kama COP31.
“Tumeingia katika kipindi kinachotawaliwa na hali mbaya za hewa duniani, hivyo tuna wajibu wa kuhakikisha tunapunguza athari za hewa ukaa na kubadili mifumo ya nishati,” alisema.
Umoja wa Mataifa, kupitia maazimio yake, inazitaka nchi zilizopiga hatua kimaendeleo, kuwajibika kwa uchafuzi wa hali ya hewa, ni imetoa afua ya kifedha kwa mataifa yaliyoathirika na uchafuzi wa hali ya hewa duniani.

















