Ulimwengu

Waziri Mkuu wa Moldova ajiuzulu baada ya miezi nane madarakani

Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya Ijumaa, Munteanu alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya “kusukumwa na misimamo yake na kile anachokiamini”.

Newstimehub

Newstimehub

3 Julai, 2026

0b1675e4d7ba4466bd9f5949bc3086fe735c4ab641f2bce0e3e51f38d7a872d1

Waziri Mkuu wa Moldova Alexandru Munteanu amejiuzulu wadhifa wake, miezi nane baada ya kukaa madarakani.

Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya Ijumaa, Munteanu alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya “kusukumwa na misimamo yake na kile anachokiamini”.

Hata hivyo, Rais wa Moldova, Mai Sandu amekana madai ya Munteanu, kuwa alikuwa akibanwa katika kutekeleza wajibu wake.

“Madai ya kuwa alidhibitiwa pale alipotaka kumbana na matumizi mabaya ya ofisi hayana ukweli wowote,” alisema Sandu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

“Alikuwa na uhuru na fursa ya kutekeleza wajibu wake ndani ya serikali.”

Kwa sasa, Munteanu atabakia kuwa kiongozi wa mpito wa ndani ya serikali, wakati Sandu akijaribu kumpata mrithi wake.