Afrika

Asasi za kiraia Tanzania zatakiwa kuzingatia sheria: Tume ya Uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura.

Newstimehub

Newstimehub

30 Julai, 2025

d62a85f647b324c060da5c7ad1fea7789e9dd5263b7bcdec077d8ca7881bd135

Taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu zimetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Tume  na taasisi na asasi hizo  leo Julai 30, 2025 jijini Dar es Salaam.

”Nitoe rai kwenu haswa wale mliopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo ya Tume wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo la kutoa elimu ya mpiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesisitiza kuwa katika kipindi cha uchaguzi Tume itafanya kazi kwa karibu na taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura.