Afrika

CAF yasogeza mbele michuano ya WAFCON 2026

Michuano hiyo, ambayo ilikuwa ifanyike kuanzia Machi 17, 2026 nchini Morocco, sasa imesogezwa mbele mpaka Julai 25, 2026, huku yakitarajia kukamilika Agosti 16, mwaka huu.

Newstimehub

Newstimehub

5 Mechi, 2026

22c83d2e22d33aadff63f88d53c921a80a3ac5b3a7ffa64e1bf7fa3244dd0cec

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa upande wa Wanawake (WAFCON 2026) imeahirishwa rasmi, kufuatia majadiliano kati ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), FIFA na wadau wengine wa mchezo huo pendwa duniani.

Michuano hiyo, ambayo ilikuwa ifanyike kuanzia Machi 17, 2026 nchini Morocco, sasa imesogezwa mbele mpaka Julai 25, 2026, huku yakitarajia kukamilika Agosti 16, mwaka huu.

Mwezi Februari mwaka huu,mjumbe ndani ya Bunge la Afrika Kusini Peace Mabe, alinukuliwa akisema kuwa Afrika Kusini imechukua nafasi ya Morocco kama mwenyeji wa michuano hiyo.

Hata hivyo, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni wa Afrika Kusini, Gayton McKenzie, alikana taarifa hizo, akisema ni bado mapema kuzungumzia suala hilo.

Idadi ya timu zinazoshindana katika michuano hiyo imeongezwa hadi 16 kwa mara ya kwanza, ambapo Nigeria ndio mabingwa watetezi baada ya kunyakua kombe katika mashindano ya 2024, yaliyofanyika mwaka jana baada ya kuahirishwa pia.