Afrika

DRC yaripoti maambukizi zaidi ya 6,000 ya Ebola yaliyothibitishwa

Tangu mlipuko huo kutangazwa mwezi Mei, maambukizi ya Bundibugyo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,900 nchini DRC, kulingana na mamlaka za afya.

Newstimehub

Newstimehub

31 Agosti, 2026

ee38fd32 5b3d 42df 8e6e c99cdb8a8755 1788198038290

Maambukizi yaliyothibitishwa ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamepita zaidi 6,000 siku ya Jumatau huku mamlaka zikiongeza juhudi za kukabiliana na mlipuko huo, takwimu rasmi zinaonesha.

DRC imeripoti maambukizi 6,041, ikiwemo vifo 2,911, tangu mlipuko huo ulipotangazwa katikati mwa mwezi Mei, kulingana na Wizara ya Afya kuhusu hali ilivyo sasa.

Watu wasiopungua 1,366 wamepona, ilhali wagonjwa 619 wametengwa au wako hospitali.

Mlipuko wa sasa wa Ebola nchini DRC ni wa pili kwa ukubwa duniani kwa maambukizi yaliyorekodiwa, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Maambukizi

Mlipuko huo, uliosababishwa na virusi vya Bundibugyo, yameathiri maeneo 60 ya afya katika mikoa sita: Haut-Uele, Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Bas-Uele na Tshopo.

Juhudi za wizara hiyo zimeendeleza kuimarishwa katika maeneo yenye maambukizi mengi, huku mkoa wa Ituri ukiangaziwa zaidi, kutokana na kuwepo kwa maambukizi mengi na maeneo ya afya yaliyoathirika.

Kuongezeka kwa maambukizi katika kipindi cha miezi mitatu iliopita kumetajwa kuwa “kiwango kikubwa” kwa maambukizi, kulingana na WHO.

Serikali imeanzisha chanjo ya Ebola ikilenga zaidi wahudumu wa afya.