Rais Recep Tayyip Erdogan aliwapokea familia na jamaa wa Hind Rajab katika Ikulu ya Rais jijini Ankara, huku pia akizungumza kwa njia ya mtandao na ndugu ambao hawakuweza kuhudhuria. Hind Rajab aliuawa Januari 29, 2024, baada ya gari la familia yake kulengwa kwa risasi na jeshi la Israel walipokuwa wakikimbia mashambulizi kaskazini mwa Gaza. Mwili wake ulipatikana baada ya karibu wiki mbili. Tukio hilo limeibua hisia za kimataifa na limeelezwa pia kupitia filamu Sauti ya Hind Rajab, iliyooneshwa kwa mara ya kwanza mbele ya familia yake katika ikulu ya rais.
CHANZO: TRT Afrika










