Ulimwengu

Iran yakana madai ya kuwa na mtambo wa Nyuklia

Kauli ya Iran inakuja baada ya Rais Donald Trump wa Marekani, kutishia kushambulia eneo la kati ya nchi hiyo.

Newstimehub

Newstimehub

22 Julai, 2026

18d0984f 633d 459d ba9b ecf79b4e18f0 1784735069417

Serikali ya Iran imepinga madai kuwa inamiliki kisiri, mtambo wa nyuklia katika eneo la Mlima Kolang.

Kauli ya Iran inakuja baada ya Rais Donald Trump wa Marekani, kutishia kushambulia eneo la kati ya nchi hiyo.

“Marekani ina shauku ya kutaka kufahamu kinachoendelea katika eneo hilo, wakati ambapo hakuna chochote kinachoendelea, ni madai yasiyokuwa na ukweli wowote,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei kupitia mtandao wa X, siku ya Jumatano.

Baqaei, alisisitiza kuwa shughuli za Nyuklia za Iran, zinatambuliwa na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).

Haya yanajiri siku moja, baada ya Rais Trump kuionya Iran kuwa, ingefanya shambulizi katika eneo la Mlima Pickaxe.