Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Son-hui amesema kuwa, nchi hiyo itaendelea kuzalisha silaha za kinyuklia kwa wakati wote.
“Kama Waziri wa Mambo ya Nje, niwaambie wazi kuwa tutaendelea kutengeneza silaha hizi, na hatutobadilisha maamuzi yetu,” shirika la habari la Korea (KCNA) likimnukuu waziri huyo.
Msimamo huo unakuja baada ya Korea Kaskazini kufanya majiribio ya makombora kadhaa, kupima uwezo wake.
Makombora hayo, yana uwezo wa kulenga shabaha za umbali wa kufikia kilomita 100.

















