Afrika

Maafisa wa forodha Kenya kujifunga kamera mwilini kama njia ya kupambana na rushwa

Mamlaka ya Mapato ya Kenya inasema kamera hizo zitazuia ufisadi na picha zitasaidia pakubwa katika kutatua tofauti zitakazojitokeza.

Newstimehub

Newstimehub

10 Mechi, 2026

dd3d0d46d0816e240076e198ace8fecfffeb643c84e1c0f1aa5bdfc80a43cf51

Kenya imeanzisha utaratibu wa kujifunga kamera kwa maafisa wa forodha na mipaka ili kusaidia kuwezesha usafiri na biashara halali, mamlaka ya mapato imesema.

Kamera 350 tayari zimepelekwa katika maeneo ya mipakani na zina lengo la “kuwezesha usafiri na biashara halali”. Kenya ni nchi iliyoendelea kiuchumi Afrika Mashariki na ina Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) – moja ya viwanja vilivyo na shughuli nyingi barani Afrika.

Mamlaka ya Mapato ya Kenya inasema kamera hizo zitazuia ufisadi na picha zitasaidia pakubwa katika kutatua tofauti zitakazojitokeza.

“Wakati kamera inafanya kazi, lazima mtu awajibike; ndivyo ilivyo. Wakati inaporekodi mazungumzo inaimarisha viwango vya kila mtu anayehusika,” mamlak ilisema siku ya Jumanne katika taarifa.

Inakuja huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ulaji rushwa kwa wafanyakazi na njama ambazo zimelaumiwa kwa watu kukwepa ulipaji kodi, vyombo vya habari nchini humo viliripoti.

“Dhamira yetu ni kuwa na usawa. Dhamira yetu ni kuhakikisha kuna uadilifu. Na tuko tayari kuwajibishwa kwa hilo,” mamlaka hiyo ilisema.

Kamera hizo zimeunganishwa na kifaa cha GPS, ambacho kina uwezo wa kurekodi matukio na kupeperusha mubashara, kulingana na taarifa za vyombo vya habari.