Mahakama ya ajira ya Paris imeiamuru PSG kumlipa Kylian Mbappé zaidi ya dola milioni 70 kwa mishahara na posho ambazo hakulipwa. Mahakama ilibaini kuwa klabu hiyo ilikiuka mkataba kwa kushindwa kulipa mishahara ya miezi mitatu, posho ya maadili na bonasi ya kusaini mkataba, muda mfupi kabla ya mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid.
CHANZO: TRT Afrika












