Afrika

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake

Bol Mel aliteuliwa mwezi Februari mwaka huu kama mmoja kati ya mamakamu 5 wa urais nchini humo.

Newstimehub

Newstimehub

12 Novemba, 2025

1990ce04b841b8febd310f224ef1d862a4256872cebc6ff99ae0c9cf87410310

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amemfuta kazi makamu wake Benjamin Bol Mel siku ya Jumatano.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo amemvua Bol Mel nafasi ya uongozi wa chama tawala nchini humo.

Uamuzi huo umemfanya Bol Mel, ambaye alikuwa akitajwa kama mrithi sahihi wa Rais Salva Kiir, kupoteza nafasi ya juu ya Ujenerali ndani ya jeshi la nchi hiyo, na kwa sasa atakuwa afisa wa kawaida ndani ya jeshi hilo.

Bol Mel aliteuliwa mwezi Februari mwaka huu kama mmoja kati ya mamakamu 5 wa urais nchini humo.