DRC yaendelea kuongoza kwa ubora wa soka Afrika Mashariki

Kulingana na takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hivi karibuni, taifa hilo linashika nafasi ya 61 ulimwenguni, ikiwa ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Newstimehub

Newstimehub

11 Julai, 2025

4520730f283a2030a3628670ffb3f9897992dbab2ad5e2e38efd965e80b30cb6

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inashika nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kulingana na orodha ya FIFA iliyotolewa Julai 10, 2025, DRC ni ya 61 kwa ubora, kati ya mataifa 210.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, Uganda ni ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki, baada ya kupanda hadi nafasi ya 88 duniani huku Tanzania, nayo ikipanda kwa nafasi nne, hadi nafasi ya 103 duniani, na hivyo kuwa ya tatu kwa ubora Afrika Mashariki.

Kenya ni ya 109 ulimwenguni, na ya nne kwa ubora Afrika Mashariki, wakati Rwanda ni ya tano, baada ya kushika nafasi 127 duniani.

fe6aba5e20f76f8efbfc8e17dc2c1ce825a8df7f10632fde7777bf3b380fca98 1

Burundi ni ya sita kwa ubora, ikifuatiwa na Sudan Kusini huku Somalia ikishika mkia, ikiwa katika nafasi ya 200 ulimwenguni.

Kwa upande mwingine, mabingwa wa dunia Argentina wameendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika orodha hiyo, huku Morocco ikishika nafasi ya kwanza kwa upande wa bara la Afrika, ikifuatiwa kwa karibu na Senegal iliyo katika nafasi ya 18 duniani.

d2237ef2523c056f139c273104ccc42aec1c094cd58e6d69f6de34b30f5fcdc4 1