Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imetangaza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga imefanikiwa kuzuia na kuharibu droni sita zilizokuwa zikielekea mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo, tukio hilo lilitokea Ijumaa jioni huku vikosi vya ulinzi vikichukua hatua za haraka kulinda anga ya taifa.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati mvutano ukiendelea kuongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati.
CHANZO: TRT Afrika














