Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amekutana na Mwanamfalme Mohammed bin Salman mjini Riyadh kujadili kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na maeneo mapya ya ushirikiano. Mazungumzo yao pia yalihusisha masuala ya usalama wa Bahari Nyekundu, eneo muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. Afwerki aliwasili Saudi Arabia Jumanne kwa ziara rasmi.
CHANZO: TRT Afrika














