Afrika

Shirika la Afya Duniani (WHO) lathibitisha maambukizi ya kirusi cha Hanta

Shirika la WHO lilisema siku ya Jumanne, kuwa linaendelea kufanya mawasiliano na mgonjwa mmojawapo aliyesafiri na meli hiyo Aprili 25, 2026, kati ya Saint Helena na Johannesburg.

Newstimehub

Newstimehub

5 Mei, 2026

a8f790ce2572d302ede70c60692f8469485721bcd34daf08507cbe44d178ffca

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha maambukizi mawili ya virusi vya Hanta kati ya watu waliokuwa ndani ya meli ya kitalii huko Cape Verde.

Kulingana na WHO, watu wengine watatu wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Shirika la WHO lilisema siku ya Jumanne, kuwa linaendelea kufanya mawasiliano na mgonjwa mmojawapo aliyesafiri na meli hiyo Aprili 25, 2026, kati ya Saint Helena na Johannesburg.

“Kufikia Mei 4 mwaka huu, maambukizi mapya ya ugonjwa huo yameripotiwa, ikiwemo vifo vya watu watatu, mmoja akiwa na hali mbaya kwa sasa,” lilisema shirika hilo.

Ugonjwa huo uliripotiwa wakati wa safari meli kutoka Ushuaia nchini Argentina kuelekea Cape Verde.