Afrika

Tanzania kufungua ubalozi Angola, kuanzisha safari za anga

Rais wa Angola, João Lourenço, yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Newstimehub

Newstimehub

29 Oktoba, 2026

7cad72d3 1fe3 41f6 9056 d5ea7e9d2e0b 1793279793740

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema nchi yake itafungua tena ubalozi wake nchini Angola kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kuongeza ushirikiano katika sekta za biashara, uchumi na uwekezaji.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Oktoba 29, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Angola, João Lourenço, ambae yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Amesema hatua inayofuata ni kuteuliwa kwa balozi atakayesimamia ushirikiano kati ya mataifa hayo.

Katika hatua nyingine, Tanzania na Angola zimesaini mkataba wa huduma za usafiri wa anga utakaowezesha kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kati ya nchi hizo, hatua inayolenga kukuza biashara, utalii na shughuli nyingine za kiuchumi.

Viongozi hao pia wamejadili namna ya kushirikiana katika kuunga mkono juhudi za kutafuta amani katika maeneo mbalimbali yenye migogoro Kusini mwa Afrika.