Nigeria inasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua shambulio la kigaidi la usiku katika kambi ya jeshi Jimbo la Zamfara, kuwaua washambuliaji kadhaa pamoja na kuwaokoa raia tisa waliokuwa wametekwa nyara.
Kwa mujibu wa maafisa wa jeshi, vikosi vilivyokuwa chini ya Sekta 2 wakiwa kwenye operesheni FANSAN YAMMA “waligundua kuna uhasama pale magaidi walipopenya kwenye kizuizi cha kambi usiku.”
Wanajeshi wakakabiliana kwa “uwezo ulioratibiwa, na nguvu kubwa,” kusababisha mapigano makali yaliyofanya washambuliaji kuachana na mashambulizi na kukimbia.
Kuwaokoa waliotekwa
“Kufuatia mapigano ya awali, wanajeshi zaidi walifika na kuwafuata magaidi waliokimbia, ambao walikuwa wameteka nyara wakazi kutoka jamii za karibu wakati wa mashambulizi hayo,” jeshi lilisema katika taarifa.
Juhudi za wanajeshi zilisaidia kuwaokoa wakazi 9 waliokuwa wametekwa, ambao walipatikana wakiwa salama, taarifa iliongeza.
Jeshi pia lilikanusha uvumi kuhusu kuuawa kwa maafisa sita wa usalama kwenye shambulio hilo, likisema kuwa “mwanajeshi mmoja pekee na polisi mmoja ndiyo waliouawa.”
Jeshi limeeleza kuwa shambulio hilo lililotibuliwa kama hatua nyingine muhimu katika kukabiliana na magaidi,” likieleza kuwa ilikuwa wikiendi mbaya kwa makundi yenye silaha.

















