Afrika

Wakenya waliohamishwa kutoka Iran wawasili nyumbani

Raia hao ambao walikuwa wanaishi nchini Iran, walipitia nchini Uturuki kabla ya kuwasili Kenya.

Newstimehub

Newstimehub

22 Mechi, 2026

5864452bf6eea85de982345ec0f2d4afc80b982692a562413d4da498a0801e81

Raia 15 wa Kenya waliohamishwa kutoka Iran kutokana na mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati, walifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumapili asubuhi.

 Kundi hilo lilipokelewa na maafisa kutoka Idara ya Nchi ya Masuala ya Diaspora.

Raia hao ambao walikuwa wanaishi nchini Iran, walipitia nchini Uturuki kabla ya kuwasili Kenya.

Serikali ya Kenya imepongeza ushirikiano wa kidiplomasia kutoka Uturuki na Iran ambao umewawezesha raia hao kufika salama.

Punde tu baada ya kuwasili, walipewa ushauri nasaha na usaidizi wa kisaikolojia ili kuwasaidia kukubaliana na hali halisi.

Baadae waliungana na familia zao zilizokuwa zinawasubiri.