Ulimwengu

Wanafunzi wa Korea Kusini matatani kwa ‘kuvunja’ na kuingia ndani ya kambi ya kijeshi ya Marekani

Wanafunzi hao, wanaume wanne na wanawake wanne, wanadaiwa kuingia ndani ya kambi ya jeshi la anga la Marekani, iliyoko karibu na jiji la Seoul.

Newstimehub

Newstimehub

4 Agosti, 2026

af6ca772 a279 480a 9ee0 36d6b10f06c6 1785851374664

Wanafunzi nane wa Korea Kusini wametiwa nguvuni baada ya kudaiwa kuingia kinguvu ndani ya kambi ya kijeshi ya Marekani.

Wanafunzi hao, wanadaiwa kutoa maneno yenye kuidhihaki Marekani, wakati wa tukio hilo.

Wanafunzi hao, wanaume wanne na wanawake wanne, wanadaiwa kuingia ndani ya kambi ya jeshi la anga la Marekani, iliyoko karibu na jiji la Seoul.

Kulingana na polisi wa nchi hiyo, wanafunzi hao wanadaiwa kupiga kelele za “kuishambulia Marekani”, wakati wakitekeleza tukio hilo.

Kwa upande wake, taarifa ya jeshi la Marekani inadai kuwa wanafunzi hao walijaribu kutumia lango kuu la ngome hiyo yenye ulinzi mkali.

Jeshi la polisi la Korea Kusini, limesisitiza kuwa, suala hilo litashughulikiwa kwa kuzingatia sheria za Marekani na Korea Kusini.