Ulimwengu

Wanafunzi warejea mashuleni baada ya vita kumalizika Iran

Hatua hiyo, inafuatia kusitishwa kwa shughuli za masomo nchini Iran, toka kuanza kwa vita hivyo, Februari 28 mwaka huu.

Newstimehub

Newstimehub

23 Septemba, 2026

ba44e87a 9c72 43e1 9743 47f9dad41740 1790170083952

Wanafunzi nchini Iran, wameanza kurejea mashuleni siku ya Jumatano, baada ya kumalizika kwa vita katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mapema Jumatano, wazazi wengi, waliwasindikiza watoto wao kuelekea shuleni, mara baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa masomo.

Hatua hiyo, inafuatia kusitishwa kwa shughuli za masomo nchini Iran, toka kuanza kwa vita hivyo, Februari 28 mwaka huu, ambapo wanafunzi 120 walipoteza maisha yao, baada ya shule moja kushambuliwa kusini mwa mji wa Minab.