Afrika

Watu 80 wamefariki dunia nchini Kenya katika ajali za barabarani ndani ya siku nne

Kenya imerekodi vifo 2,933 vya barabarani kufikia sasa mwaka wa 2025, huku vifo 80 vimeripotiwa katika muda wa siku nne zilizopita, amesema Waziri wa Barabara na Uchukuzi Davis Chirchir.

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

471560bdf8025c427f80f449004a365a66b2619c94ed36a245a78eac9bfd4700

Kenya imeshuhudia moja ya wikiendi mbaya zaidi mwaka huu, kufuatia msururu wa ajali zilizoshuhudiwa nchini humo.

Chirchir alisema Wizara yake imezindua “ukaguzi wa usalama” nchini kote na ukaguzi katika sehemu za barabara zinazokabiliwa na ajali ili kubaini hatari, kujenga upya barabara kwenye maeneo ya ajali, na kuja na mapendekezo ya kiufundi ndani ya siku saba.

Waziri huyo aliongeza kuwa mageuzi ya sheria yako katika hatua ya juu zaidi ili kuimarisha sheria za usalama barabarani haswa katika usafiri wa shule, uendeshaji wa magari ya biashara, madereva walevi, ukaguzi wa magari, vituo vya kando ya barabara, na mapitio ya Sheria ya usalama barabarani.

Waziri huyo vile vile amesema Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) itaongeza kampeni ya kutoa elimu kwa umma ili kuhimiza matumizi salama ya barabara.