Ulimwengu

Zelenskyy adai watu wa karibu wa Putin wanataka vita vimalizike

Kiongozi huyo wa Ukraine anadai kuwa Urusi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta kwa kushindwa kumaliza vita

Newstimehub

Newstimehub

10 Julai, 2026

4a6770ff d58d 427e a94d dc4023e5258a 1783714015298

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema kuwa sehemu ya watu wa karibu wa Rais Vladimir Putin wa Urusi wangependa kuona vita kati ya mataifa hayo mawili, inafikia kikomo.

Akizungumza siku ya Ijumaa, Zelenskyy amesema kuwa, kwa sasa Urusi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati ya mafuta kutokana na kugoma kumaliza vita hivyo.

 “Tumekuwa na mapendekezo ya namna ya kupata amani, tumeungwa mkono na washirika wetu wengine pamoja na watu wa karibu wa Putin,” alisema kiongozi huyo.

Hata hivyo, Urusi haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya Zelenskyy.