Serikali ya kijeshi ya Mali imewakamata majenerali wawili na raia mmoja wa Kifaransa kwa tuhuma za kuvuruga amani nchini humo, chombo cha habari cha Mali kimesema.
Vyanzo mbalimbali viliieleza Reuters kuwa zaidi ya wanajeshi 30 walimetiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na uvuragaji amani nchini Mali.
Kati ya waliokamatwa, ni pamoja na raia wa Ufaransa, aliyetambulika kama Yann Vezilier.














