Afrika

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaifutia Somalia deni la miaka 38

Somalia imeishkuru Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ikieleza uamuzi huo kuwa mafanikio ya ”kihistoria”.

Newstimehub

Newstimehub

2 Septemba, 2025

59fa571c9620555084bd0f3dcda45ac2147e462f86b1d6593e37e2f2d3139998

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeifutia deni la asilimia 75 Somalia kwa kile Balozi wa Somalia nchini Misri na Mwakilishi katika Jumuiya hiyo, Ali Abdi Aware, ameeleza kuwa mafanikio ya ‘‘kihistoria’’.

Balozi Aware alihutubia mkutano wa 164 wa Wawakilishi katika Jumuiya hiyo siku ya Jumanne mjini Cairo.

Alitoa shukrani za Somalia kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na wanachama wake kwa kuunga mkono Somalia kuomba kufutiwa deni ambalo limekuwepo kwa miaka 38 lililotokana na kutolipa ada ya uanachama.

Jumuiya hiyo iliidhinisja kufutwa kwa asilimia 75 ya malimbikizo ya deni, Shirika la Habari la Somalia, Somali National News Agency limeripoti.