Afrika

Luhaga Mpina: Sirudi CCM ng’o

Mwanasiasa huyo, ambaye uteuzi wake wa kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ulitenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), amesema kuwa hana nia ya kurejea kwenye chama chake cha CCM.

Newstimehub

Newstimehub

3 Septemba, 2025

43b34550100f80314c72205b8569b2f1d9181d24434b47a9585c46940c874b3a

Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo cha nchini Tanzania, Luhaga Mpina amesema hana mpango wowote wa kurejea kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza Septemba 3, jijini Dar es Salaam, Mpina ambaye uteuzi wake wa kugombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo ulitenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo (INEC), amesema kuwa hana mpango wa kurudi ‘nyumbani’, licha ya ombi lililotolewa na mgombea Urais wa CCM, Emmanuel Nchimbi.

“Nimesikia wakizungumza kule jimboni kwangu, oooh, Mpina rudi CCM, nyumba ipi…nishasema sitorudi CCM, nimeondoka CCM, sitorudi CCM,” alisema mwanasiasa huyo na mbunge wa zamani wa jimbo la Kisesa.