Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametetea hatua za vyombo vya ulinzi na usalama wakati wa machafuko ya Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa nguvu iliyotumika ilikuwa muhimu kulinda amani na kuzuia jaribio la mapinduzi. Katika mkutano na wazee wa Dar es Salaam, Rais Samia aliashiria kwamba baadhi ya makundi yaliyochangia vurugu hayo yalikuwa na nia ya mabadiliko ya kisiasa kwa nguvu, na kutahadharisha kuhusu shinikizo la kigeni linalolenga rasilimali za Tanzania.
Rais alionya kwamba Serikali imejipanga kuzuia maandamano yanayotarajiwa Disemba 9, 2025 na wakati wa sherehe za Krismasi, akisisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuendeleza umoja na kulinda amani. Pia alifafanua kuwa madai ya kisiasa, ikiwemo mchakato wa mabadiliko ya Katiba, hayapaswi kutumika kama sababu ya kuvuruga nchi.














